KISWAHILI 1 VTP

Husika na Muhtasari wa somo la Kiswahili I – COS121 - A/Y 2017-2018;

Yaani yaliyomo (Course contents)

Kwa kiwango hiki kinachohusu MAFUNZO YA UFUNDI /VTP, mambo muhimu yafuatayo yametiliwa mkazo kwa madhumuni ya kuwasaidia wanafunzi kuwasiliana na wengine katika Lugha ya Kiswahili, ndani ya ulimwengu huu wa Teknolojia na Ufundi; hususani watakapokuwa uwanjani wa kazi.

-      Maamkizi

-      Nafsi na Matumizi ya nyakati

-      Sarufi Maumbo (Maneno na matumizi yake katika sentensi)

-      Sarufi Miundo (Sentensi na matumizi yake katika mikutadha tofauti)

-      Kusoma (matini mbalimbali) na Ufahamu

-      Dhana / Maoni kuhusu Fasihi (Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi)

-      Ujuzi wa mawasiliano

-      Msamiati mbalimbali:

 -Jamaa,-Nyumbani, -Vifaa vya ufundi, -Wanyama, ndege na wadudu, - Mimea na  

  miti, - Kazi mbalimbali za watu, - Viungo na sehemu za mwili, - Kuhesabu   

  (Hisabati) na wakati (saa)

 

-        Mazoezi kuhusu:

. Majadiliano kupitia mazungumzo mbalimbali, midahalo, mijadala, michezo …ili   

  mwanafunzi aweze kujieleza bila hofu /wasiwasi na kukamilisha ustadi wake katika lugha  

  ya Kiswahili. Mada tofauti zimechaguliwa.

. Kufikiri kwa kina (Critical thinking) ili Mwanafunzi aweze kutoa mawazo na maoni  

  yake kuhusu jambo fulani na kujieleza imara mbele ya wenzake, darasani. Jambo hili 

  litasisitiziwa katika makundi.

. Utungaji wa Mazungumzo (Dialojia) utasisitizwa kwa madhumuni ya kusaidia  

  wanafunzi kusema kwa ufasaha Kiswahili sanifu; kupitia mazoezi ya

 - kutunga sentensi sahihi kisarufi, kamilifu na zenye mantiki.

 - Kuboresha lugha kwa kutumia ishara zinazoambatana na mawazo pamoja na hisi.

 

                               Mhadhiri KAYIRANGA THEOBALD.


MODULE TEAM: KAYIRANGA Theobald